One The Incredible - Rap Science lyrics

Published

0 323 0

One The Incredible - Rap Science lyrics

(VERSE 1) Hii ni news kwa ma – rap star/ Kwenye mdundo mi ni bao, nateleza na nina ujuzi wa kunata/ Utunzi bado culture, na – peruz kurasa/ Mwenyeji vituo vyote kama mluzi wa kondakta/ Uhh.. Beat ya Den texas/ Nchi ya verse, tenzi hazihesabiki hata kwa census/ Sense sick, spit ka` na – desease kwa senses/ New era muzik, Old rapper hit the benches/ Nawakilisha illmatix toka enzi/ Ikiwekwa beat kati tunagawa kama chenji/ Peace kwa J ryde, Bano Stylez enzi Toka tunafanya freestyle kwa ringtone za dre beats/ Tenzi za roho kutoka kwa rap dayosis/ Niko sick, sitibiki kwa anti-biotics/ Maabara ya mziki na – deal na rap science/ Uno the Chemist, Niko na text the Mad scientist… (VERSE 2) Check…. Hii ni for the people wa kitaa, People wa mitaani/ The people behind bars wanaoishi kwa imani/ Mother kani – teach tuko equal so sidhani…./ …. Ka` nikiku – treat sivyo tutakuwa people wa amani/ Sikupeleki higher nakurusha/ Haina ku – retyre, weka fire kama kaya kwa wavuta/ Namwaga dawa ka` supplier, ama pusher/ Mpaka wanachoka mbaya, shonea waya kwenye bukta/ Mbaya nawakilisha/ Hata nibarikiwe na uhai wa kujidai mpaka Messiah anapofika/ Na sina ubaya, nimeutumia mpaka umekwisha/ So, hata niki – retyre nitaimba kwaya ya kanisa/ We ni Big screen star unaetisha/ Mi ni sixteen bars za sifa, hapa u – star unakwisha/ Muda hausimami, masaa yanapita/ Maisha ni movie ya kila siku, mi ni star kwenye picha… (VERSE 3) Hii sio Hip Hop conscious, ni hoja njema/ Sina nguzo tano, mi natumia moja vyema/ Moja tena, niite nyota njema/ Ka` ulie nae mikosi huna budi kumngoja Mwema/ Bado mbinde nilinde hali/ Mkali jilinde, kama unaringa kibingwa karinge mbali/ Jilinde na zali, habari zifike kwa wahuni wa maskani, niko nanyi kama vizinde vya kali/ Sina drama wa beef kumbuka/ Hizo peleka kwa baby – momma, sio sisi utaumbuka/ Huu ndo mwanga, mweusi hawezi wanga, hapa zina twangwa chungu sio rahisi kumumusa/ Ukihisi nimekugusa, Diss/ Hizi flo kubwa zinawavuka, iwe bukta ama jeans/ Stuka ama sizi/ Sanuka hawa machizi wameshafua, na hawawezi kukauka zama hizi…