Nikki Mbishi - Utamaduni lyrics

Published

0 739 0

Nikki Mbishi - Utamaduni lyrics

Verse I: Yo, vina punch na midundo, mafumbo na temithali Za semi, zisome tungo, ni gumzo, jiweke mbali Mi ni fundo we ni mwali nishike udumishe ndoa Bila mishe niko poa nipishe nisafishe doa Nadharia kwa kilinge, ninge hazitambi tena Nishinde mbilinge, Mungu hazijui dhambi njema Gongo La Mboto msoto hainyweki gongo ya moto Maisha vitisho, mwisho wanaujua hadi Mrisho Mpoto Kafara za kuchinja fake wanachimba Kila napo timba wanapotea ki mazingara kama ninja Choir master bubu, rasta choma kaya, fire Si husudu mabaya, hii ni saa mbaya, muhaya tubu Napanga mistari mithili watoto wa kaya za kipemba Mashairi ka riwaya za Andanenga Nafunza kwa Kilingi Kama tenzi ni hela ubongo wangu ni benki, so nazitunza ka shilingi Blow kiss kama jada, makada ndio sisi We radar police, snitch vipi unidiss bila mada? Wonder kama Stevie na hii flow ndiyo yenye mwali Inayokubamba kama mwizi na siku hizi Emcees hawalali Hook: Ni Utamaduni, au sio, sio mbio za sakafuni Japo umefichwa kapuni ka siri ya mafanikio Shika kanuni za majilio Nani abuni jipya, chini ya jua ni marudio Au sio, sio mbio za sakafuni Japo umefichwa kapuni ka siri ya mafanikio Shika kanuni za majilio Nani abuni jipya, chini ya jua ni marudio Verse II: Bashiri unavyoweza, au beza inapostahili Au tabiri kama pweza, jeneza linamsubiri Na eneza mashairi mithili ya injili ya ebeneza Kiswahili, kiingereza nacheza mahiri naweza Nawapa somo wana, bila kikomo nachana Media zinabana promo, na mdomo bado umeachama Katuni tupa kapuni, na kupa kanuni Supa kapuka hazivumi, shtuka, zinduka na utamaduni Mbishi ni oversize, nivae nikuvuke We ni mayonnaise kwenye mkate, ngoja uchakae baadae wakutupe Ndani ya kilinge nitinge, chui ni vimbe We hujui mbinde, Msondo huijui ngoma ya sikinde Na survive na vibe za live bendi Mi na mengi ya ku-describe, sio pride ya ku-drive range Hii ni wazi, nina hadhi ya wako role model Na sio stori ndogo, ka una maradhi twende loliondo We ni James Bond toy, mi ni James Bond mtu Wanarespond, lecture ka za Desmond Tutu Siyo choo cha kike, hiki ni choo cha mashoga Sina uoga napo flow, na hii siyo show ya mapouka Hook: Ni Utamaduni, au sio, sio mbio za sakafuni Japo umefichwa kapuni ka siri ya mafanikio Shika kanuni za majilio Nani abuni jipya, chini ya jua ni marudio Au sio, sio mbio za sakafuni Japo umefichwa kapuni ka siri ya mafanikio Shika kanuni za majilio Nani abuni jipya, chini ya jua ni marudio Verse III: Hakuna dili itafanyika, bila kuweka pesa mob Nipe job ya uhakika, ni show ka nesta bob Na rob akili zenu kwa rhymes, beat na flow Unadata kisha unafyata ile time sh** inablow 9-1-1 DANGER, emergency call Mbona game imejaa ma-stranger, hii siyo basketball Uwe tall, alafu unamudu ma-slum dunkin' Au Elvis Presley, King wa Jam Funky Mi ndio actor, wa movie isiyo na scripty Macho kwenye paper, michuzi uzi kwa snitchy Mistari mijeledi inachapa kisha inachana Akili ingekuwa nywele wenye dread wangeshindikana Na design mbinu za kuwaibia, ka Fundi Frank Pesa taslimu, haina cha skonyo za hundi benki Bongo bwana, huwezi kukuta magaidi jela Bali wezi wa kuku ka chege wa saidi fella Swing dozen, chini nna buti kali Bitozi na mapozi, mitaani hutafuti ugali Mida mibovu, so mbishi nna skuti mbali Street hukuti mwali, bali ni species za __ Hook: Ni Utamaduni, au sio, sio mbio za sakafuni Japo umefichwa kapuni ka siri ya mafanikio Shika kanuni za majilio Nani abuni jipya, chini ya jua ni marudio Au sio, sio mbio za sakafuni Japo umefichwa kapuni ka siri ya mafanikio Shika kanuni za majilio Nani abuni jipya, chini ya jua ni marudio