Nikki Mbishi - Natoka Tanzania lyrics

Published

0 644 0

Nikki Mbishi - Natoka Tanzania lyrics

Intro: Ngwessa Natoka Tanzania (Yea,yea Natoka Tanzania) Yea, Tamaduni Muzik baby (Wakilisha) Unju bin Unuki (nchi yetu TZ Bongo) Naipenda Tanzania (Jamani karibuni tufanye utalii wa ndani au sio...) Yea 1,2 1,2 We don't stop til' the music... (..wanyama wapo mtaani siku hizi hawakai mbugani tena) Verse I: (Yea) Nchi ambayo haithamini mchango wa sanaa Wanaoitwa wasanii, mitaani wanakufa njaa Bongo fleva ni utumwa Ndiyo maana machizi wanajituma kusukuma madawa ya kulevya (wanyama) Tony Montana, Noriega Pesa motivator, nicheki kwa Sony Wega Nchi ambayo, stori ndogo ni gumzo kwa taifa Nguza, Papii Kocha jela kifungo cha maisha (aiyaa) Nasema ukweli, tindikali si hofii Wezi wa rasilimali za serikali wako free Wako hai kimwili, kiakili wameshakufa Hata hoja fupi wataijadili hadi kesho kutwa Nchi ambayo, mpaka mortuary wanaomba rushwa Traffic na dereva, polisi yuko kwa pusha Wako ghetto wana moka cha Dom na cha Arusha Na ukiongea umbea tu, umesutwa! Hook: Ayo, Natoka Tanzania, TZ Bongo Nchi ambayo Viongozi wana-CV za uongo Asilimia 70, wananchi ni maskini Kaa chini fanya tathmini, niambie unacho ona nini Natoka Tanzania, TZ Bongo Nchi ambayo Viongozi wana-CV za uongo Asilimia 70, wananchi ni maskini Kaa chini fanya tathmini, niambie unacho ona nini Verse II: Nchi ambayo, Raisi ni mzito kwenye maamuzi Anafumbia macho vigogo na walanguzi Vya msingi nyuma, vya mbele ni vya kipuuzi Na juzi, alikuwa kwenye msiba wa Bongo movie Nchi ambayo, falsafa hazina tafsiri Kwenye shule za kata hakuna mtoto wa waziri Tunasoma sisi tu Tunazidi ku-potezwa mithili fisi ndani ya misitu Mashabiki wanapenda flow za Nikki Wanahoji vipi? mbona si sikiki, tuzo hamnipi Nikidiss wanasema natafuta kick Nchi ambayo 50 Cent an*lipwa mimi silipwi Kama unapeta, peta ila jichunge Ukitaka kuwa Shetta nenda kwa Chief Kiumbe Nchi ambayo ma-meneja ni ma-damager Eti, trap beats ndiyo kipenzi cha ma-teenager Hook: Ayo, Natoka Tanzania, TZ Bongo Nchi ambayo Viongozi wana-CV za uongo Asilimia 70, wananchi ni maskini Kaa chini fanya tathmini, niambie unacho ona nini Natoka Tanzania, TZ Bongo Nchi ambayo Viongozi wana-CV za uongo Asilimia 70, wananchi ni maskini Kaa chini fanya tathmini, niambie unacho ona nini Verse III: Tanzania, wala si msanii jamani Kama ni uzalendo tuanze na utalii wa ndani Nchi ambayo sista du hajui Emcee ni nani Field Marshall nawachora ma-MP vitani Nijenge nikujenge, tujenge na tupendane Siyo una-like fan page yangu ili unitukane Au nifanye kama Dimpoz nadai Nikate mauno, Rich Mavoko, bolingo nangai Nchi ambayo wawekezaji imewabidi kusanda Mashoga kibao, Bongo umagharibi umetanda Sababu ya joto, hasira inazidi kupanda "Stay Positive" aliniambia Fareed Kubanda Karibuni Tanzania, Wazungu, Walatino Wa-Dutch, Wazulu, Waarabu, Wafilipino Toka Ukonga ya Ilala, Temeke wapi Kino Na ukitaka Ganja kali ni Sinza kwa Cappacino Hook: Ayo, Natoka Tanzania, TZ Bongo Nchi ambayo Viongozi wana-CV za uongo Asilimia 70, wananchi ni maskini Kaa chini fanya tathmini, niambie unacho ona nini Natoka Tanzania, TZ Bongo Nchi ambayo Viongozi wana-CV za uongo Asilimia 70, wananchi ni maskini Kaa chini fanya tathmini, niambie unacho ona nini Outro: Yea, Niambie unacho ona nini Nikki Mbishi Baba Malcom Unju bin Unuki, Zohan, ?? Baba Bomba, Utingo tishio Jogoo Majina Kibao, nipo na Ngwessa au sio Hii ndio ile nchi bwana Shabiki ana-like fan page yako Facebook Anaku-follow twitter, instagram ili akutukane sio Badala ya kukushauri akujenge Sikilizeni nyie, ukitoa maisha ya kwenye media Tuna maisha binafsi pia Kwa hiyo tusifwatiliane kupita kiasi ,au sio Ehh, hii dunia tu, Dunia njia Na dunia ni gunia, na gunia halibebi maji Au sio, Ahsantee