Nikki Mbishi - Michepuko lyrics

Published

0 191 0

Nikki Mbishi - Michepuko lyrics

Intro: Yea, Michepuko Ngwessa (Huh) Kinyee, Zohaan Yea, Unju bin Unuki [Verse I: Nikki Mbishi] Huwa nasikiasikia tu Eti niache michepuko na milupo ili nibaki njia kuu Napenda nitulie ndani ya ndoa Nihudumie familia watoto wajisikie poa Ila, mke wangu ndiye kikwazo Kila ukizuka ugomvi basi ujue yeye ndiyo chanzo Washikaji wananiita bwege hamnazo Mademu kibao, kwanini mmoja anitie mawazo Kila siku napiga magoti Nyumbani ka vitani, huyu mke au field force? Maana makofi nayo naswa ni kiboko Tena mbaya zaidi napigwa mbele ya watoto Siwezi kuongea neno moja Maana ashajazwa umbea, na wambea ni mashoga Basi atafura, mezani siachiwi hata chakula Kulala mzungu wa nne amekunja sura Asubuhi mida ya kwenda kazini Hapigi pasi, haniwekei maji huwezi kuamini Namtazama simmalizi Mpaka najiuliza nani ananipa script kwenye drama kama hizi Najiuliza mi ni Mume au Mlinzi? Maana usiku kucha nakesha ka' Jinamizi Hajawahi nifanyia fumanizi Na kila nikiondoka namwachia pesa ya matumizi [Hook: Kinye Wynjones] Tusilaumiwe tu kuchepuka, nimelazimika, jogoo kuwika tu Kwenye kila ovu kuna force(noma) Tusilaumiwe tu kuchepuka, nimelazimika, jogoo kuwika tu Kwenye kila ovu kuna force, noma [Verse II: Nikki Mbishi] (Yea) Na ndio maana naona bora kuchill Na malaya kwenye club, labda watanifeel Stress anazonipa mke wangu zitanik** Ingawa nampenda sana, yea nampenda for real Utanikuta Corner Bar, mezani nyama choma imezagaa Pembeni nimezongwa na vifaa Bila hofu, mifuko wananichuna Pedeshee Nikki, michepuko ni sunna Siku hizi imeshakuwa kasumba Ndoa kuvunjika, uhusiano wa mapenzi kuyumba Mpenzi wako akikuita special, jua kuna mtumba Uchawi pesa, hakuna cha tunguli wala ndumba Mfatilie demu wako upate BP Kazi tunayo sisi magazeti na TV Mwanamke haridhiki, sa sijui anataka nimpe kipi Ama, anataka nimpe kiti Kwenye moyo anikae nijae Niishi naye, kama juzi, sasa mpaka baadae Nje ya ndoa siende kwa makusudi Ila mke wangu amezidisha mauudhi Japo nabugi, lakini sina budi Jogoo wangu anawika na panga langu si dubi Kwanini na chepuka na ulevi? Miaka mingi imepita, mpenzi wangu hajawahi kuniita baby (and i real miss that, real miss that) (Eh, hayo ndio mapenzi au sio, lets go) [Hook: Kinye Wynjones] Tusilaumiwe tu kuchepuka, nimelazimika, jogoo kuwika tu Kwenye kila ovu kuna force (noma) Tusilaumiwe tu kuchepuka, nimelazimika, jogoo kuwika tu Kwenye kila ovu kuna force, noma Tusilaumiwe tu kuchepuka, nimelazimika, jogoo kuwika tu Kwenye kila ovu kuna force (noma) Tusilaumiwe tu kuchepuka, nimelazimika, jogoo kuwika tu Kwenye kila ovu kuna force, noma