Nikki Mbishi - I’m Sorry JK lyrics

Published

0 2056 0

Nikki Mbishi - I’m Sorry JK lyrics

Hook x 2 It will one day make sense Nikisema hakuna president kama JK Tanzania inakumiss yaani daily Kwa niaba ya wabongo i’m sorry JK Verse 1 I’m sorry JK nimeona tu niseme Mzuka huu niliupata nikiwa Juu Kijenge Mikopo hakuna tena huendi chuo kikuu kizembe Bungeni wan*lewa wanabonga tu king’eng’e Wakitwanga wanatamba wakisanda wanatubu Simuoni tena Jay tangu akutane Sugu Scorpion amegeuka ghostface mwema Aliyeota Rais atakufa anaitwa Godbless Lema RC na Wasafi uswazi madefender Hapa Kazi tu mtaani njaa kali sio sinema Kama kuisoma tushaisoma namba/Ungegombea awamu ya tatu ingekuwa bora labda Hook x 2 It will one day make sense Nikisema hakuna president kama JK Tanzania inakumiss yaani daily Kwa niaba ya wabongo i’m sorry JK Verse 2 Enzi za bibi cheka wengi walikuita babu cheka Hawakujua kuwa nyakati zinakuja nakusepa Ulivunga wakibeza kuwa unapenda sana bata Na kiki ka” Makonda za Wasafi kuwafuata Wabongo watakumbuka kwenye sekta ya michezo Mpaka Taifa Stars nayo ikaonesha mauwezo Ukaongeza vigezo nyenzo matengenezo Leo Samatta ndo kinara na hachezi soka la dezo Tuzungumze magazeti Bunge wanaedit Hakuna mikakati bwana kumbe wanaekti Demokrasia demoghasia za Field Force Wengi wanafear ukweli kuwaambia Unju siogopi Mabenki yanafilisika madeni yanamimika Hali imekuwa ngumu hadi wageni wanasikitika Hatusheshi na shisha yaani sio fresh inatisha Bar mwisho saa sita siku hizi hatukeshi kabisa Hook x 2 It will one day make sense Nikisema hakuna president kama JK Tanzania inakumiss yaani daily Kwa niaba ya wabongo i’m sorry JK Verse 3 Kila taarifa ya habari leo JPM Pesa imepotea kimazingara David Blaine Waathirika hawaelewi juu ya mipango ya Bukoba Tetemeko wasije kula michango ya Msoga Tumekosa usitupe laana tucorrect Weka kando chama tuwe wana tuconnect Hela imefichwa nyuma ya Pazia la viwanda Njoo Sogodo uone Tanzania ya vibanda Uone chafu moja na askari mia wakisanda Chocho za Panya Road mixer pwiya la miganja Kuna nyakati nilikudiss JK Now I’m calling for the peace,DAMN! We miss JK Hook x 2 It will one day make sense Nikisema hakuna president kama JK Tanzania inakumiss yaani daily Kwa niaba ya wabongo i’m sorry JK