John B - PAMOJA NASI lyrics

Published

0 774 0

John B - PAMOJA NASI lyrics

INTRO Emmanuel Mungu pamoja nasi Ndani ya rohoo wako anahitaji nafasi VERSE Neema yake Mungu ndio taa ya Wokovu Nijaze ni we mkamilifu niachane na uovu Kwakupigwa kwake Yesu tumepona Uponyaji unaohiotajika niwewe kumpokea Kutii ni bora kuliko sadaka Aimaanishi ndio mwisho wa wewe kutoa zaka Neno lake liko hai litende ndio uponyaji Sauti ya Bwana ni amri na roho wake ndiye mpaji Yesu asipokutumia ufanyalo utendalo utenda bure Mkombozi ndiye njia auhitajiki uende shule Haya ya moyo wako nia ya kuacha utu wa kale Kusudi la mbingu latimia ni wewe kuwa mteule Kumpenda Yesu neno lake kuliishi Ndani ya Kristo ndio uzima wetu, kila mtu anao huo wito Emmanuel , mungu pamoja nasi Nuru ya Roho mtakatifu Msaidizi, mtetezi Na hii ndio ahadi itokayo juu.. VERSE Heshima, utajiri na dhahabu vyote vyake Hauna budi ye kumkiri,penye bonde ubebwe Ukimuamini neon ni dira , ulisome usibweteke Ufunua mambo ya fumbo na siri, uyajua gizani na nuru ukaa kwake Moyo wako ukiwa safi yesu anagawa vipawa Umtoa mtu mavumbini, kwa uhaminifu unao tawala Usitumike na shetani kama mlango watenda baya Nyenyekea ukitubu kwa yesu usione haya Rohoni kujiandaa, kila leo tuna hubiri Kanisani , mtaani kwenye njia Sikia sauti hii, ushindi tumepewa kwa msalaba calvary Matendo ya mwilini ndo njia pana ya motoni Matunda ya rohoni njia nyembamba ya uzimani CHORUS Emmanuel , mungu pamoja nasi Nuru ya Roho mtakatifu Msaidizi, mtetezi Na hii ndio ahadi itokayo juu.. VERSE 03 Nakuita rabi , mwalimu, mzabibu wa kweli Umenifanya niwe mwanga nawe ni nuru ya ulimwengu Nimepata wokovu kwa neema sio zali Pia umenipa hiyo haki kwa ukiri wa kinywa change Nakuhitaji unilee mwenyewe sintoweza Asante kwa upendo malaika zako uninilinda Mwili uikana roho, roho uvumilia nakushinda Matendo yako ya ajabu ninao ushuhuda Nafsi iliruhusu mwili nakunipa mchanganyo Nilikuwa mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo Hofu mashaka wasiwasi vilinitisha Lakini roho wako leo amenihuhisha Nakuita aba yan baba Mimi ni motto nakutii mwenye mamalaka, heshima na uwezo CHORUS Emmanuel , mungu pamoja nasi Nuru ya Roho mtakatifu Msaidizi, mtetezi Na hii ndio ahadi itokayo juu.. Emmanuel , mungu pamoja nasi Nuru ya Roho mtakatifu Msaidizi, mtetezi Na hii ndio ahadi itokayo juu.. OUTRO Gelax wakristo.....william kipemba Isaiah 61;1 This is my logo