Masebo - Niachie Mimi lyrics

Published

0 253 0

Masebo - Niachie Mimi lyrics

[Intro] Yoh yoh, R City baby, Hazard, Masebo Shah-Beezy, Shah Bang, Tarakimu, Salmin Swaggz [Verse 1: Salmin Swaggz] Huu ni mgodi wa madini makini kuniskiliza Huyu ni Salmini huamini au unajiuliza Anaimbaga nini mi naona kama huaga anaigiza an*leta story na swagger za Tambwe Hiza Nilianza kufoka kabla hata hujaanza kukaa Hujui nlikotoka unadata na Jeans niliyovaa Watu walishoboka kabla hatujatoka kitaa Siku hizi nmeacha kumoka mtaani wameshaichoka bidhaa We “street certified” kitaa kishatupa ridhaa Kila mahala kuna ghala la kuficha silaha Mi naongoza huu msafara bila babu na Slaa Imani haiko kwenye sala tunahesabu masaa Niulize mimi, ka demu wako akitaka kuaachiwa ulimi Muulize, je ni yakini anataka kuachiwa UKIMWI? Dhiki baraka kwangu unataka uniambie nini Game ni kibaraka wangu ukishindwa niachie mimi… [Hook: Shah Bang & Tarakimu] Yako tatu, yako mbili ila moja…niachie mimi Nenda mgambo, sungusungu, u-soldier…niachie mimi Una hoja ya nguvu, mi nna nguvu ya hoja Wa mbili havai moja utangoja…niachie mimi (Repeat) [Verse 2: Shah Bang] Bora uniachie urithi wa Amani moyoni mwangu Sio matamanio ya kijinga yaathiri maisha yangu Usiniachie UKIMWI japo nna pesa ya kuhonga Usiniachie mademu japo nna uwezo wa kugonga-nisha Gla** za wine, it's time to shine Uzuri sio umbo ni tabia na hulka Skiza hizi tungo ujiepushe na ufuska Niachie bili ya uzima mi ndo ntailipa Utukufu wa roho mbinguni mambo yatajipa Niachie rap niachie chap I'm in top Niachie mimi niwaulize waliofeli walijiandaa Au kile walichosoma wizara ilikikataa Uchakavu wa maisha kitaa, ni mazoea Dhambi ya mlalahoi ni story ya babu Seya Mbegu waliyoipanda tayari imekwisha stawi Taaluma hazifanya kazi ila kutafutana kwa uchawi.. [Hook: Shah Bang & Tarakimu] Yako tatu, yako mbili ila moja…niachie mimi Nenda mgambo, sungusungu, u-soldier…niachie mimi Una hoja ya nguvu, mi nna nguvu ya hoja Wa mbili havai moja utangoja…niachie mimi (Repeat) [Verse 3: Tarakimu] Niachie mimi, bingwa wa biashara Ambaye najiamini, na naipinga hasara Mjasiria mali niliyejawa ubunifu Kila saa niko tayari kukabili kila kitu Niachie utafiti, nikupe matokeo Nna mbinu ya kudhibiti uhaba wa pembejeo Nina uthubutu, akili sio butu Natumia mawazo, mtaji na sio mtutu Najua bidhaa, bei, banda na bango Daima sikosei nimejipanga kitambo Hua naficha mia kila nikipata mia mbili Hakika nimepania mpaka waniite tajiri Nakopa kwa fursa, nalipa kwa wakati Naogopa kuvaa Supra, riba itanish**aki Ukipata kidogo bwa'mdogo acha dharau Maisha yakikupa kisogo chap tutakusahau [Hook: Shah Bang & Tarakimu] Yako tatu, yako mbili ila moja…niachie mimi Nenda mgambo, sungusungu, u-soldier…niachie mimi Una hoja ya nguvu, mi nna nguvu ya hoja Wa mbili havai moja utangoja…niachie mimi (Repeat)