Chorus: Hili joto hasira, ambaa Upepo hakuna Ambaa, naruka mwenyewe Yelela, yelela, ambaa. Foleni njia nzima, ambaa Na pesa hakuna Ambaa, naruka mwenyewe Yelela, yelela, ambaa VERSE 1: Kila siku nimenuna Kwanini tunagombana Tena tunakosoana, kama tumechanganyikiwa Na sioni hata maana Ya si kuzinguana Yaani kila mtu anajua sana Au yote sababu ya?, sababu ya? Rudia Chorus: VERSE 2: Mazao twalima wote Sahani wavuta kwako Kama chakula tule wote Kwanini chote kije kwako Kisu mpini umeshika wewe Vitisho kunikata mimi mmmmhh Au yote sababu ya? Sababu ya? Chorus: Hili joto hasira, ambaa Upepo hakuna Ambaa, naruka mwenyewe Yelela, yelela, ambaa. Foleni njia nzima, ambaa Na pesa hakuna Ambaa, naruka mwenyewe Yelela, yelela, ambaa Hook: Uuuuh, sahau sahau shida Oooh ishi ka ziliisha jana Say goodbye joto, Rest in Peace Shida Knock, knock money RAP: Wenyewe wanasema usawa unakaba Na rafiki wa kweli ni mama na baba Hawa wengine wala usiwaamini Maana binadamu wa sasa wana roho saba Watakuwa na wewe kwenye raha Na hawatakuwa na wewe kwenye njaa Bora nipige misele yangu peke yangu Niruke kivyangu na woga niliukataa Aaah!! Nabadilika kama saa Na Siku hazigandi na sitokataa tamaa Wamejaa, usaliti na chuki Watu wa karibu wanageuka mamluki Jenero nasonga iwe joto au baridi naamini tutashinda Kama mbwai iwe mbwai barida We make more money rest in peace shida Ukinuna unataka tunune wote Ukilia unataka tulie wote Vita vyako tunapigana wote Tukishinda tushinde au bora tufe wote Kama kulima kote tumelima wote Hata kupanda kote tumepanda wote Kupalilia tumepalilia wote Aaaargggh !!! nashangaa sasa mbona hatuvuni wote?? Chorus: Hili joto hasira, ambaa Upepo hakuna Ambaa, naruka mwenyewe Yelela, yelela, ambaa. Foleni njia nzima, ambaa Na pesa hakuna Ambaa, naruka mwenyewe Yelela, yelela, ambaa