Izzo Bizness - BARAKA lyrics

Featuring ,

Published

0 1205 0

Izzo Bizness - BARAKA lyrics

ilianza kama ndoto na si masihara/ Kuna time ilipita hata bila ya kula/ Hatukusikitika tulishukuru kwa mola/ Na kila baya tulilizuia kwa sala (Amen)/ Mama Baba walishikana wakavumilina/ kuna mifano tunaiona wengi tu wanaachana/ inapoingia shida dhiki hufarakana/ Maugomvi kila siku mwisho wanatengana/ Tukapiga moyo konde tukasema ipo siku/ Kwa zuri baya hatukuacha kamwe si kisifu/ Maana matatizo tumeumbiwa Sisi watu/ Kukufuru ni makosa hairuhusiwi katu/ Nyumba tuliyopanga migogoro kibao/ Mwenye nyumba anataka alipwe yake mafao/ Na baba kodi hajapata tutafanya nini leo/ Kote tupu bila bila hakuna kimbilio/ Kuna siku nakumbuka yani noma mzee/ Mama alinipigia and she was crying aisee/ Anasema wanadharaulika sana kisa kodi/ Ananiombea kwa MUNGU afanye wepesi ikibidi/ Look leo I made it/ Nimemjengea Mama/ Yes n***a I did it/ Hakuna stress tena/ kiaina yeee we spend it/ Tunafurahi sana/ Zile tabu I can't forget it/ Zilitutesa sana yeee… Chorus: Kwa BARAKA za wazaziiiiii Kwa kuwajali wazaziiiiii Kwa BARAKA za wazaziiiiiiiiiiiii (Nimetoboaaaaaaaaa) Kwa kuwajali wazaziiiiiiiiiii (Nimetoboaaaaaaaaa) July 4 nimetimiza malengo Nimeacha wazazi wanaishi kwenye mjengo… Kuimba kwangu sio kama nazuga Nafanya mziki mkali ili nitimize malengo X 2 Verse:2 Ni furaha ilioje leo mnyamwezi mii natamba/ Mama na Baba yangu leo wanamiliki nyumba/ Miaka thelathini na moja nyumba za kupanga/ Leo wako Huru kwao haki kujigamba/ Namshukuru MUNGU katenda miujiza/ Kwa kunipa imani na kuamini nitaweza/ Kwa kufanikisha huu Mkate juu ya meza/ Tumesamehe wote wale wote waliotubeza/ July 4 elfu mbili kumi na tano/ Furaha ya ajabu yee pasipo mfano/ Machozi ya furaha nikajikuta tu nalia/ Mama anapiga simu mwanangu leo tunahamia/ Mateso ya nyumba za kupanga walichoka/ Walihamia pasipo nyumba kukamilika/ Madirisha hakuna,sakafu vumbi linatimuka/ Baridi ya Mbeya nadhani ushaipata picha/ Nawashukuru wadau wa hii sanaa/ Na mashabiki wote kila kona ya mtaa/ Ma dj,ma presenter sijawatupa jamaa/ July nne jumapili nyota njema iling'aa/ Look leo I made it/ Nimemjengea Mama/ Yes N* gga I did it/ Hakuna stress tena/ Kiaina yee we spend it/ Tunafurahi sana/ Zile tabu I can't forget it/ Zilitutesa sana yeeeee… Chorus: Kwa BARAKA za wazaziiiii Kwa kuwajali wazaziiiiii Kwa BARAKA za wazaziiiiiiiiiiii (Nimetoboaaaaaaaaa) Kwa kuwajali wazaziiiiiiiiiiiiiii (Nimetoboaaaaaaaaa) July nne nimetimiza malengo Nimeacha wazazi wanaishi kwenye mjengo Kuimba kwangu sio kama nazunga Nafanya mziki mkali ili nitimize malengo X 2 Outro: (Nature) Hutuchomi Muhindi kwa tochi Kiganja cha sokweeeee Vatete va kuntanzaniiii Hizi raha za Tanzanianoooo Izzo Biznengaaaa Hiiii Hiiiiiiiiiiiii Kama kalambwandaaaaaaaaaa…….