Erick Wainaina - Daima Kenya lyrics

Published

0 9566 0

Erick Wainaina - Daima Kenya lyrics

Verse 1 Umoja ni fahari yetu Undugu ndio nguvu Chuki na ukabila Hatutaki hata kamwe Lazima tuungane, tuijenge nchi yetu Pasiwe hata mmoja Anaetenganisha Chorus Naishi, Natumaini, Najitolea daima Kenya, Hakika ya bendera Ni uthabiti wangu Nyeusi ya wananchi na nyekundu ni ya damu Kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani Daima mimi mkenya Mwananchi mzalendo Verse 2 Kwa uchungu na mateso Kwa vilio na uzuni Tulinyakuliwa Uhuru na mashujaa wa zamani Hawakushtushwa na risasi au kufungwa gerezani Nia yao ukombozi kuvunja pingu za ukoloni Chorus Naishi, Natumaini, Najitolea daima Kenya, Hakika ya bendera Ni uthabiti wangu Nyeusi ya wananchi na nyekundu ni ya damu Kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani Daima mimi mkenya Mwananchi mzalendo Verse 3 Wajibu wetu Ni Kuishi kwa upendo Kutoka ziwa Mpaka pwani Kaskazini na kusini Chorus Naishi, Natumaini, Najitolea daima Kenya, Hakika ya bendera Ni uthabiti wangu Nyeusi ya wananchi na nyekundu ni ya damu Kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani Daima mimi mkenya Mwananchi mzalendo