Ender - Kemosabe lyrics

Published

0 330 0

Ender - Kemosabe lyrics

Niliamini mapene hayatoshi..na niki-hustle siyakosi/ Sababu.. sipo kwenye loss na life simple huwa hai-cost/ Kwahivyo nikaenda Dar na treni... of thoughts../ Sikwenda kuzubaa au kushangaa nikusaka chapaa boss/ Sikutaka kuivaa mikosi..nilitaKa kuivaa mikoti/ Sikuwa na pa**port..pa**word.. pin..lakini ni crack codes/ Walionisapoti wote siwaoni kwa line/ Wakini-approach ili nifungue pochi ya noti tu-shine..hatuko fine/ Je mimi ni kaka mubaya...? kaka aso haya../ KAKA..? huniitaga NAKAAYA/ Mama C huniita brother bila shaka.. Mozaya/ Niko sick & tired of being sick & tired/ Na huu ni mwaka wa ndui/ Sitaki upele urudi tena.. mnachotaka sikijui/ Nashukuru hamtopata mbawa ikiwa mtaupata huo uchui/ Mnautaka uadui? mnayempaka ni mtata.. makaka hamkui? Mmeendekeza hila.. legeza hasira za harakati/ Mie nita-ball.... hata kwa mpira wa makaratasi/ Unaweza ukahisi mie napita tu.. kwakusahau mie nina-hustle/ Nimezaliwa Afrika.. ugumu wa maisha umenifunza ku-struggle/ Ukiwa idle.. unamu-attract shaytwan (SHETANI)/ Kichwani nina MSAHAFU na BIBLE.. life ni zaidi ya ku-have fun/ Kwani.. Kila kicheche anajiona ni mzima/ Na njia pekee ya kuepuka ngoma ni kugoma kupima/ Ikiwa maujuzi haya hayakugusi.. itanilazimu nikuelewe/ Sometimes hata kamusi.. huimiss tafsiri yenyewe/ Nalindwa na dua za mama.. tangu baba simjui/ Namfanya adui mwenye njama aache drama na akue/ Ili ajijue kabla hajakwama huko mrama asitue/ Ajikwamue kwenye lawama.. yenye maana yamchukue/ Kisha anaiombee mimi ili nifaidike kwa hizi mbio/ Siamini kwenye umasikini hivyo sihofii mafanikio/ Ndiyo.. mie ni LEO kwahiyo sifikirii kushindwa/ Zingatia kauli hiyo hausikii inaashiria ubingwa?/ Mie ni mbishi.. muulize Nikki - hatopinga/ Na hata kama ningekua mbuzi ningelala chaka la simba..