INTRO
Emmanuel Mungu pamoja nasi
Ndani ya rohoo wako anahitaji nafasi
VERSE
Neema yake Mungu ndio taa ya Wokovu
Nijaze ni we mkamilifu niachane na uovu
Kwakupigwa kwake Yesu tumepona
Uponyaji unaohiotajika niwewe kumpokea
Kutii ni bora kuliko sadaka
Aimaanishi ndio mwisho wa wewe kutoa zaka
Neno lake liko hai litende ndio uponyaji
Sauti ya Bwana ni amri na roho wake ndiye mpaji
Yesu asipokutumia ufanyalo utendalo utenda bure
Mkombozi ndiye njia auhitajiki uende shule
Haya ya moyo wako nia ya kuacha utu wa kale
Kusudi la mbingu latimia ni wewe kuwa mteule
Kumpenda Yesu neno lake kuliishi
Ndani ya Kristo ndio uzima wetu, kila mtu anao huo wito
Emmanuel , mungu pamoja nasi
Nuru ya Roho mtakatifu
Msaidizi, mtetezi
Na hii ndio ahadi itokayo juu..
VERSE
Heshima, utajiri na dhahabu vyote vyake
Hauna budi ye kumkiri,penye bonde ubebwe
Ukimuamini neon ni dira , ulisome usibweteke
Ufunua mambo ya fumbo na siri, uyajua gizani na nuru ukaa kwake
Moyo wako ukiwa safi yesu anagawa vipawa
Umtoa mtu mavumbini, kwa uhaminifu unao tawala
Usitumike na shetani kama mlango watenda baya
Nyenyekea ukitubu kwa yesu usione haya
Rohoni kujiandaa, kila leo tuna hubiri
Kanisani , mtaani kwenye njia
Sikia sauti hii, ushindi tumepewa kwa msalaba calvary
Matendo ya mwilini ndo njia pana ya motoni
Matunda ya rohoni njia nyembamba ya uzimani
CHORUS
Emmanuel , mungu pamoja nasi
Nuru ya Roho mtakatifu
Msaidizi, mtetezi
Na hii ndio ahadi itokayo juu..
VERSE 03
Nakuita rabi , mwalimu, mzabibu wa kweli
Umenifanya niwe mwanga nawe ni nuru ya ulimwengu
Nimepata wokovu kwa neema sio zali
Pia umenipa hiyo haki kwa ukiri wa kinywa change
Nakuhitaji unilee mwenyewe sintoweza
Asante kwa upendo malaika zako uninilinda
Mwili uikana roho, roho uvumilia nakushinda
Matendo yako ya ajabu ninao ushuhuda
Nafsi iliruhusu mwili nakunipa mchanganyo
Nilikuwa mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo
Hofu mashaka wasiwasi vilinitisha
Lakini roho wako leo amenihuhisha
Nakuita aba yan baba
Mimi ni motto nakutii mwenye mamalaka, heshima na uwezo
CHORUS
Emmanuel , mungu pamoja nasi
Nuru ya Roho mtakatifu
Msaidizi, mtetezi
Na hii ndio ahadi itokayo juu..
Emmanuel , mungu pamoja nasi
Nuru ya Roho mtakatifu
Msaidizi, mtetezi
Na hii ndio ahadi itokayo juu..
OUTRO
Gelax wakristo.....william kipemba
Isaiah 61;1
This is my logo