Tazama Sasa tunasherehekea upendo wetu
Mapenzi tele siwezi kuelezea
Bila hiyana bwana karuhusu tupendane
Bila hiyana ameruhusu upendo kwetu
Mmh
Tumepewa silaha mbali mbali za maisha
Uaminifu,amani,upendo nayo heshima
Ikawe siku njema kwako mpenzi wangu
Ikakufariji hii nyimbo na kukuliwaza.
Chorus1:
Nibembeleze mpenzi
Mapenzi tele nipatie
Usiruhusu mpenzi
Linikute baya Mimi
Aah
Upendo wako usiugawe kwa mafungu
Nipe upendo wote kwani Mimi Ni wako tu
Nipet pet nipe mahaba Moto Moto milele
Nikiss kiss nipe mapenzi yaan Kama mtoto
Chorus2:
Unifariji milele
Nikwazikapo my boo
Wee ndiye wangu laazizi
Nipe lake penzi my boo
Tabasamu lisilokauka nigeie
Penzi lisilonyauka milele nilipate
Watoto Kama wote Mola atujalie
Pokea nyimbo hii popote ulipooo Aaah