Verse 1
Mcheza bongo Mac Muga
Yuko single sana Mac Muga
Ukimwona mtu akijinamia kwa sababu ya
maisha yamchanganya Chali wangu alizamia
Kuenda kusini mwa Africa Huku pia akimchanua kwa sababu ya maisha aliyofuma Alikuwa maarufu sana, Akajiona yeye ndo winner Kwa kujichanganya na wasichana Club zote za huko kujulikana
Yeye Mac Muga Wewe Mac Muga Ah,
hii dunia, Mac Muga huruma!
Chorus 2x
Mungusha asumani alipofika South Africa
alikuwa na maisha bora Ya juu,
ya thamani tena yanayohitajika magari yote
kwa nyumba Mbona sasa amesharejea,
hajui wapi ataanzia!
Hakuna kazi mtu akajinamia
Mac Muga hii ni dunia
Verse 2
Akajichezea,
gari ya kutembelea Shida walimwelezea wasichana
na shida zao akawatatulia
Wewe upewe nini Mac Muga
Mungu akupe nini Mac Muga?
Nyumba ulijijengea,
foro kuta nyumba Wewe ndio wewe,
wengine fala! Wewe,
Mac Muga Mbona sasa umeshatimua!
South Africa wamekutimua
Na sasa home usharejea
Wewe Mac Muga Mungu akupe nini Mac Muga?
Chorus 2x
Mungusha asumani alipofika South Africa
alikuwa na maisha bora Ya juu,
ya thamani tena yanayohitajika magari makubwa,
nyumba Mbona sasa amesharejea,
hajui wapi ataanzia Hakuna kazi mtu akajinamia
Mac Muga hii ni dunia!
Verse 3
Yipes kana huoni kwa Mac Muga
Woi noma huruma kanyongo'nyea
Afanye nini sasa,
cha kufanya Kila anachachofanya anaona anakosea
Yikes,
kama huoni kwa Mac Muga Woi noma huruma kanyongo'nyea Afanye nini sasa,
cha kufanya Kila anachachofanya anaona anakosea
Akiwa jambazi akili zake zitaishia
Akiwa mwizi anaona atauliwa
Akifikiria kujiua Nafsi yamzusha basi an*lia
Wewe Mac Muga! Mungu akupe nini Mac Muga?
Wewe Mac Muga! Basi upewe nini Mac Muga?
Mungu alikuzawadia Sasa ushachezea!
Wewe Mac Muga ! Basi upewe nini Mac Muga?
Mungu alikuzawadia maisha Sasa ushachezea!
Haya, haya, Wangu Mac Muga
Msela hao Wa mpani huna Wasee wa maskani wanakukimbia! Mac Muga noma Hee!
Mac Muga Skonde, upige moyo konde,
Mac Muga!