Fid Q - Ni Hayo Tu lyrics

Published

0 542 0

Fid Q - Ni Hayo Tu lyrics

Intro: Oyaa, dogo, we mshamba we njoo hapa We ndio wanakuita Fid Q, (Ndio) Hebu atupe mistari kwanza... [Verse I: Fid Q] Korombwea hayo maisha ya kuungaunga, hiyo shughuli mi naiweza Hapa utaambulia ushauri ukihitaji msaada wa kifedha Mi kujiita rasta, wenye chuki tu wanapinga Wanashangaa na kula nyama, hawajui nyota yangu ni ya simba Asiye fikiri kabla ya tendo, atatendwa pale akidamka Na usinidiss kwa kiswahili kama hujui hata kukitamka Kuongea sio kusema na kufumbua macho sio kuamka Wasiwasi ukiwanyima raha, mistari itawafanya kuchangamka Mnapagawa na baadhi ya mambo ambayo nayajua Pia nna uwezo kufanya mpaka madawa yanaugua Hii ni I level, sio high level ndio maana hunioni Waulize wenzako, Fid Q yupo juu zaidi yako homie Nipo juu, je utanibana kama kizibo cha soda? Kushuka ngazi tu unahema, je kuzipanda hupati uoga? Amini usiamini, Fid Q ndiyo sauti ya mtaani Je, mtafurahi nikishuka chini kama mademu wa marubani Bora kuogopwa, wakikupenda watakuchukia Nilipo na nilipo anzia, sipo napo hitaji nibaki pia Si hofii kupitwa ilimradi muda usiniache Hii ni kwa wote, popote Siogopi kuomba mvua najua mnayahofia matope Mwingine anakurupuka ananiiga, anasema sifai Naona vibaya kumjibu, sahau kutupa mawe juu ya mayai Chipukizi chapeni kazi ili mng'atuke mlipokwama Vumilieni kama nyota mtatoka jua likizama Ni binadamu sijakamilika, kuandika rhymes sikosei Japo miluzi ni mingi lakini jibu huwa sipotei Nitaendelea kuwa mshindi wa juu ka majani na record Bongo Nakutembea kifua mbele utadhani nimedundwa ngumi ya mgongo (Aargh, Fid Q kitu gani bwana...) (Afu mi ananikeraga anajifanya anapenda mademu wa kizungu) (Achana nae, nyie asikuzingueni Bongo fleva kitu gani...) [Hook: Fid Q] Kila mtu Fid Q hivi, mara Fid Q vile Yaani Fid Q, Fid Q, Fid Q tuuu, ni hayo tu Kila mtu Fid Q hivi, mara Fid Q vile Yaani Fid Q, Fid Q, Fid Q tuuu, ni hayo tu [Verse II: Profesa Jay] Ukinicheka shambani, mi nakucheka sokoni Chuma au fua chuma, ni mwendo wa roho mkononi Maisha ni mpangilio, ukitulia yanajiseti Ni kama A to Z kwenye mfumo wa alfabeti Hawara hana takala, ukimtaka unampata Bendera ibaki hewani, natimba chaka kwa chaka Hatufanani kama alama za vidole Na bado naziamini falsafa za mwenda pole Unaishi nyumba ya vioo, basi usinitupie mawe Heshima yangu sikuipata katika sandakalawe Inakuwaje unadiss? unampaka wa mawazo Unazungumzia ujazo, milazo au micharazo Nilichuna wakati wa kwenda, ila sasa narudi Nikanyage bahati mbaya nikulipue makusudi Ni hayo tu, kama hujitumi piga mihayo tu Fid Q na Jizze heshima ndiyo tuitakayo tu [Hook: Profesa Jay] Kila mtu profesa hivi, mara Profesa vile Yaani Jay profesa? Jay tuu, ni hayo tu Kila mtu profesa hivi, mara Profesa vile Yaani Jay profesa? Jay tuu, ni hayo tu (..jana nilimuona maskani, kaja na kipensi rafiki yangu Afu sijui kanywa gongo alafu ile Benzi lao an*lisukuma halina mafuta..) (We mwenyewe unamuonaje kwanza?) (..njaa.. anapenda tatizo mimamaa..) [Verse III: Langa] Natumia akili, ustaarabu, na subira Situmii mwili, jazba, na hasira Mapinduzi daima, msimamo ka Che Guevara Usingizi ndugu yake kifo, sipendi kulala Nafuata mipango yangu, sifuati mipango ya wengine Niko focused, hata ikibidi vingine nijinyime Wote tukiwa masikini, nani atamsaidia mwenzake? Niacheni ni win, majungu msinipake Wanasema nimechange, eti sio mimi wa zamani Sionekani maskani kwa darubini wala miwani Lawama kibao utadhani mahakamani Mi nisipo hangaika atayenilisha nani Wananichekea usoni, kisogoni wananisema Wanatafuta mabaya, wanjifanya hawaoni mema Kisichoniua kitanikomoza ki-askari Unavyo nichukia unadhihirisha mi mkali Sina haja ya kurudia, Fiddy alishawaambia "U-superstar mzigo wa mwiba" ukiubeba unaumia (Langa langa, langa kilanga?) (Kajinga tu kale) (..Ye mwenyewe mshamba tuu) (eti, kabosi kale, ..yaani mimi kalanga kale..) (Machizi wamemsaidia kishenzi.. wamembeba mpaka wamemchoka) (..Sio inshu yule aah sio inshu yule..) (..uhh, kichwa chenye utadhani madenge..) (na na nanilii ngoja nikwambie, unajua eti enzi zile...) [Hook: Langa] Kila mtu Langa hivi, mara Langa vile Yaani Langa tuu, yaani Langa tuu Kila mtu Langa hivi, mara Langa vile Yaani ni hayo tu, huh, ni hayo tu [Outro: Fid Q] Na nafuata njia zangu kama Carlito Nayajua mateso kama Mel Gibson na Apocalypto Na nafuata njia zangu kama Carlito Nayajua mateso kama Mel Gibson na Apocalypto