Fid Q - Siri Ya Mchezo ( The Game's Secret ) lyrics

Published

0 564 0

Fid Q - Siri Ya Mchezo ( The Game's Secret ) lyrics

Nilipotoka mbali na ninaheshimu nilipo/sikuwa na umuhimu kihivyo… stimu zikanipa elimu ya Biko/ Kimaandiko… kimistari.. hadi fans wanascream nikirap../ sikuamini kama nina zali mpaka nilipoidream hiphop/ Wanapagawa…. Na baadhi ya mambo nayoyajua.. pia nina uwezo wa kufanya mpaka madawa yanaugua/ Wanapagawa na nyimbo ngumu hawa #teamMabiiitoz / Achana na power window.. sijui rimz za dimpoz/ Haileti bingo, mshiko? Star ishi simple/ sanaa iko hivyo sometimes.. hukataa kukaaa ulipo/ Wanaodharau.. hujiletea matatizo..hawajui kama wadau… hupendelea kukuona hivyo?/ bonge la staa.. donge la njaa.. hauna kitu/ Jikombe ugongwe…mtaaa ukuone hauna ishu/ Ukishindwa kujiandaa… jiandae kushindwa/mjinga utaachwa unashangaa kumuona Martin Kadinda/ Usmati anaotinga, majumba mandinga ya bwana Almasi.. je hizi track za harakati ni ujinga?/ HAPANA.... nguvu ya mamba ni maji/ na umaarufu au kutamba.. kushika namba ni bahati..sio kipaji kama Kubanda eti unachana kigumu/ kisa track ikivuma sana kwenye chati haidumu / Amani kwa chachage na MAKUWADI wa SOKO HURIA../ baba asante kwa UTAFITI na ZAWADI ya ALMASI ya BANDIA/NYUMBANI… nasikiliza DUNIA YA SASA ya MARIJANI../ najiuliza tutarithi nini ikiwa IMANI ishakwisha tangu zamani?/ labda kubisha na wakinitisha najihami../ inasikitisha unapoibiwa na aliyekupigisha ni jirani/ ‘' Pole MAPROSOO'' ( uhujumu --uchumi ) umefanya umetubu.. / WAZEE ni wahuni hadi soo waay back before SUGU/ Taifa la kondoo.. huendeshwa na serikali ya Dubu/ na MBWA MWITU wenye siri.. ili bepari umuabudu/ kimahakama, kiserikali, kidini umsujudu../ huo ni utumwa pia/Unafanya vijana wanaumia../ Tunaishia kufia mabatani kama nzi ndani ya gla** ya bia.. CHORUS: ( Juma Nature ) Siri ya mtungi aijuaye kata../ komaa… kaza.. kisha utapata/ x 2 Siri ya mchezo naijua mimi.. tu.. na hakuna mwingine x 2 VERSE 2: Tofauti ya BIASHARA na SIASA ikila hasara inaweza buma/ wakati SIASA kila mara ukiwa unang'ara ujue kuna.. kinara/ anayeunda msafara wa wanaojituma na kuchuma kwa kukufanya uwe imara hapo hasara hakuna/ KIDUMU CHAMA CHA MASELA… Ukoloni mambo leo umetupa uhuru wa bendera,/ Tuone kufuru za wenye hela/ TANZANIA ni ‘ demu wa mtungo ‘ wanamuiita CHA WOOTE/'' HANGOVER .. ‘'anaikimbia kwa kupiga ‘ “ mtungi “ saa zote / Mkubwa anazuga atasolve… matatizo ya nchi yake/ ‘'na gari bovu..'' halisukumwi kwa kukaa ndani yake/ MAENDELEO ni ile ndoto..MWEZEKAJI ashaipuuza../ je Kukaa karibu na moto ni kuuota au kujiunguza? / hakuna UHURU wa kweli (Africa) msidanganywe na illusion/ na daily tunafeli sababu ya POLITICAL institutions/ CIVILIZATION imeadvance sasa wanatuua economically../ hakuna utumwa mbaya kama ule wa kujiona uko free/ Kuusaka ukweli ni sawa na kumenya kitunguu/ kila ganda litakutoa machozi na utabaki macho juu/Ukishafika kwenye kiini niambie nini utagundua..? zaidi ya mafaili yaliyounganika utaghairi kuyafunua? Wamejivisha U-NOAH.. SAFINA zao zikatoboka/ Wakajivisha U-MUSSA.. FIMBO zao hazikugeuka NYOKA/ Sasa wanaujaribu U-MUNGU MTU kuamua nani leo atatoka….!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!???????????????????