Fid Q - Bendera Ya Chuma lyrics

Published

0 1409 0

Fid Q - Bendera Ya Chuma lyrics

V E R S E 1: (Fid Q) Naitwa FAREED.. Kwa maana mie ni wa kipekee na wa aina yake/ Huu UJASIRI na huu UTAJAIRI WA MASHAIRI una tafsiri zake/ JASIRI coz SIOGOPI kuumia/ Nikiwa na NOTI hutumia/ Akina KIDOTI wakiniaproach huwakazia/ TAJIRI WA MASHAIRI.. Mie sio hodari wa kurap tu/ Mie sio msanii, naifanya hii kwa ajili ya watu/ Nina USO WA MBUZI.. Na ninapewa front page/ Na DAILY kwenye NEWS sina skendo yoyote/ WAPI? WAPI? WAPI? WAPI niliwakosea?/ WAPI mie siku-play fea (fair)?? Sikuzaliwa niwe KAMILI nilizaliwa niwe REAL yeaah../ Na UDHAIFU hauna DILI ikiwa ni STRONG najiFEEL here/ NADHIFU KIAKILI, STREET SMART… BLACKSHAKESPEARE/ Nipo ili nife, MAISHA sio mchezo wa UWOGA, MJOMBA/ Unataka nishibe? Hakikisha haukombi MBOGA BOMBA/ Nipake TOPE..NIJIKOMBE, NIKUOMBE MAFUTA/ UNIPONDE..UNIZONGE KUTWA,NIKONDE MNYONGE WA KUTUPWA/ Kwa MGONGO WA CHUPA nipake nisije kupauka/ Nitaibuka tu kama vumbi.. DONGO likija kukauka/ H O O K (Ben Pol) Ninateleza.. Nakosea.. Naanguka.. Napotea/ Najifunza.. Kuendelea.. Ninainuka.. Natembea/ Nateleza.. Nakosea.. Naanguka.. Napotea/ Najifunza.. Kuendelea.. Ninainuka.. Natembea/ BENDERA YA CHUMAAA.. INAPEPEA BENDERA YA CHUMA… BENDERA YA CHUMAAA.. INAPEPEA BENDERA YA CHUMA… V E R S E 2: (Fid Q) Ninachunga HASIRA isiniumize ili MAUMIVU yasinitishe/ Hawaishi HILA wenye WIVU wananizingira nisipite/ DUA haziishii ANGANI/ UA linazaa BUSTANI/ BAHATI haina AHADI ikihitaji hutua NDANI/ SIHOFII kudondoka sababu mie nina MABAWA/ Waliofikiria nitachoka.. wanaogopa.. NGOSHA ana POWER/ CHEUSI ni mzawa.. CHEUSI ana DAWA ya kutoka/ Pagawa ukinitosa.. KOSA kunawa kabla haijatosha/ Kivipi UNIACHE wakati huu MZIKI uko na mie na kwake nina MAPENZI YA MSWAKI, Sitaki mwingine achangie?/ MASIKA bila MBU.. sio GHARIKA bila NUUH/ SHIDA anazo kila MTU.. CHAKARIKA uje UNAFUU/ B R I D G E (Ben Pol ) HEKIMA ni kukosa excuse.. kukosa excuse.. unapo loose/ Na pia ukishinda usijiboost.. usijiboost.. yanini makuzi/ HEKIMA ni kukosa excuse.. kukosa excuse.. unapo loose/ HEKIMA ni kukosa excuse.. kukosa excuse.. unapo loose/ H O O K (Ben Pol) Ninateleza.. Nakosea.. Naanguka.. Napotea/ Najifunza.. Kuendelea.. Ninainuka.. Natembea/ Nateleza.. Nakosea.. Naanguka.. Napotea/ Najifunza.. Kuendelea.. Ninainuka.. Natembea/ BENDERA YA CHUMAAA.. INAPEPEA BENDERA YA CHUMA… BENDERA YA CHUMAAA.. INAPEPEA BENDERA YA CHUMA… V E R S E 3: (Fid Q) Ninawafanya wanaKAA.. kama yule MC wa Kenya/ Ukisikia PAA.. ujue haikupangwa UFE mapema/ Sikuiti SHUJAA.. kwa kufanya kile unachofanya/ Nitakuita MJINGA.. ikiwa UKISHINDWA wakati CHAWEZEKANA/ DUNIA ni kubwa pia ni ndogo kama TUKIUNGANA/ KIUTUUZIMA.. Na MLIMA haupandwi, kwa KUUTAZAMA/ Ningekua KISIWA..MAISHA yangu yangekua ufukweni/ Huu upeo NIMETUNUKIWA na MUNGU wangu basi nipokeeni/ INATOSHA? Wanasema ‘ HAPANA ‘ DONDOSHA../ Na tena wanaochana.. hawajiiti CONSCIOUS ni NGOSHAZ