Fid Q - Sumu lyrics

Published

0 517 0

Fid Q - Sumu lyrics

[Verse I:] Aliyeniumba alinipa mdomo hivo n'na haki kuongea Hii bahati meotea, safi kamwe siachi kui-share Hamtaki niwe fair, trust me man huwa happy nki-care Naona watachosema mshkaji uko smart upstairs Usiache kuongea, usiache we ni incharge huna spare Kipaji ka' Ngwair, mapaji ka' bahati aliowagea Flag pepea, hitaji zaidi ya maji na mmea Ilikuwaje wa muache hadi mshkaji ulaji wa d** ukamzoea Tunamoka ili kusafiri kihisia Au kufoka pia ikitoka ukaisikia huwezi toka au ukitose kuingia Kinachochosha nia, ni kosa ulichojua utapatia Nawachota kihisia, nasota, je inatosha fidia Shibe ya mdau hainilazi njaa sababu mganga yupo juu Nafurahi ambavyo wadau wakimuona star wan*lamba miguu Asiye nihitaji simuhitaji, kamwe simuachi aje azinzi Bandidu kama tsotsi sipigi goti ka' PNC Hakuna ambae hakosi, labda ____ kwa ______ Yangu self esteem haitoki ka' ripoti za TMZ Na hainizuii nsile mkate, kwa kuhofia kiungulia Na u-Emcee hauniachi, huniangalia ka ______ Ka' Bruce Lee hizi karate, ntakupigia utaishia Na sinto sita kusema ahsante au kuwasifia mkinisaidia Washkaji baadhi hawana haki ya kui-pressure hii medulla Wako radhi kukupa pombe na siyo pesa ya kula Nawaona vyura tu kama Snura, hii sura ya mhuni haina kwere ______ anavaa suti mtaani, nyumbani kunguni tele Kwa magonjwa yanayotibika tunapoteza maisha, Huruma Tunachanga kwenye msiba ukifa, hawajali ukiumwa Au wanaweza wakahisi umekufa kwa kukutwa umezirai Usipo sh'tuka Afrika unaweza kuzikwa ukiwa hai [Hook:] Sumu Sumu, Sumu Sumu Sumu,Sumu [Verse II:] Haumuui chura kwa kumtupa ndani ya maji Ukinizuga kwa ulaji, nakupa fact kwa lugha ya kishkaji Unataka vitu rahisi, mi' nawapa vitu halisi Utata unamtaka ibilisi, na siyo bi kaka ka' Idris Mr. Nice jua la utosi na mtaa unakiu ile mbaya Hawamsupport, isipokuwa anawapromote aliowa-inspire Wakati, ___ sio kama Mox, Stosh hakupaswa kumgwaya Lakini, mzee bila noti ni zaidi ya Nyoshi akiwa vibaya I didn't come this far, just to come this far Siwezi sanda kama bikra hata nikiishi ki-star Maisha hayakupi unachotaka ila yanakupa unachotafuta Pesa sadaka, wazushi wanaivuta kwa ________ Binadamu wako wapi mnanitoa mie nsiwemo Leo nawapa ofa ya mswaki afu kesho mnaning'oa meno Oyoooo.. time is money nafasi haijali kuzuga Wema anataka saa ya almasi zari anaujali muda Washa sana nyasi, rasta ogopa fast futa Wanashindwa kujinafasi kwa unafiki nafsi zinawasuta Wabongo wa majuu hamna upendo, mnajigawa Ubongo hauna miguu lakini skendo zina mabawa Aliyemtia umasikini Afrika leo an*lia kwa yanayomsibu Na hutangaza akimpa msaada kiasi cha kumtia aibu Dunia siyo chafu ni chafu uchafu tukiutazama Sumu ndani ya watu, na ndiyo hapohapo tunapokwama Hawaamini kwenye kuunda Diamond au Kiba wawili Wanachoamini ni kumshusha mmoja ili mmoja awe dili Cha kupewa hakishibishi ukipewa lazima ukumbushwe Dunia mwendo wa ngisi, kung'aa sio lazima star ashushwe Ukiacha hisia zikuendeshe, kwa ujeuri utaishia kufeli Sababu neno la ukweli sio zuri na neno zuri halina ukweli Ntasahau vyote, milele ntamkumbuka aliyeniumba Na daily ntakaa mkao wa pusha tu kama Umbwa