Fid Q - Bongo Hiphop lyrics

Published

0 544 0

Fid Q - Bongo Hiphop lyrics

BONGO HIPHOP VERSE 1: Ulianza wewe.. wakaja waimbaji na wabana pua/ Wale mwewe.. Franga wawindaji wakatusua/ Kwakuwa.. wanajua mshikaji unaishi kwa miko/na zako itikadi.. ziko kimziki na sio mshiko/ Kama haileti hela..basi haimake sense.. no sweat kisela mie nikakomaa tu na lako penzi/ Sikusound garbage au kuchange suddenly../ Mie ni mjeshi so naweza fight savagely/ Hiphop ya ukweli.. ukapigwa radioni/sometimes malaika wa heri nao hutembelea motoni/ Penzi ni kipofu na anayemuona halioni/ sikuwa na hofu.. mama alinipenda tangu nikiwa tumboni/ I started young.. I made my mother's womb a drum/ My umblirical chord a guitar.. muhoji aliyenizaa/ BONGOFLAVA mzuri kiasi.. hiphop we ndo my queen/ my 1st.. my last & everything in betweenjj Chorus: Mimi na wewe.. tangu long time/ Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame/ Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream… BONGO HIPHOP X2 ' VERSE 2: Kama kukupenda wewe ni dhambi.. basi shetani yu nami/ na kamwe sintonyea kambi ili niwabambe dukani/ For a million little pieces naweza kumcon Oprah ka James Frey/ Na watasema sitishi wakati wanaogopa nisitokee/ Waufuate mkumbo huu wa wasomi.. wa midundo na mistari/ ukiwa na nyundo mkononi.. ni rahisi kupigilia msumari/ Sio tu bongo.. mpaka Ng'ambo hakuna uhuru wa habari/ kuna uhuru wa mwenye chombo.. mitambo na mwenye mali/ Kujifanya hawasikii.. haiwasaidii.. wala haiwajengi/ unachosema ni.. kamwe IPP haitompinga Mengi/ Unawakumbusha wazazi wa uswazi.. chati ya uteja imeingia/ na Mapusha wanauza d** ili walishe familia/ Mbaya.. kuhifadhi fuvu la mtu ndani ya kabati/ mbaya zaidi ni kuwa na ndugu.. halafu kichwa maji/ Amka bongo lala.. hiphop sio ufala.. ni lazima uifate/ Uaminifu ni kama mshahara.. fanya kazi ili uupate Chorus: Mimi na wewe.. tangu long time/ Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream… BONGO HIPHOP X2 VERSE 3: Mapenzi ya sikuhizi.. bila kugombana yanakua hayana stimu/ Pia ni ruksa kushikana lakini sio kushikiana simu/ Inanipa wazimu.. kusikia kimwana haujaachana na Hasheem/ Na bado mnawasiliana..una mpango wa kuchanganya timu?/ Nakupenda hiphop.. ndo maana ninarap ile mbaya/ Naspit fire bila hennessy.. au kula kaya/ I want my art to be my legacy.. kabla sijaretire.. waanze nigwaya hawa enemies.. anyways NI HAYO TU/ Beef huletwa na wivu.. na wivu sio hiphop/ MC nayetaka BEEF amlete Maza ake kwa strip club/ BONGO FLAVA ananipima.. kama nimeiva kimasomo/ Anagundua mie ni dreamer pia ni believer zaidi ya Common/ Cha ajabu hunitempt... ili nikuache HIPHOP/ Anaahidi atanipa GOOD SEX.. wewe unanipa TRUE LOVE/ Hajui who's next.. wewe unanipa tu mashavu/ Nikipaa.. anaumia.. anatamani nishuke chini/ Nami sikutamani USTAA.. USTAA ulinitamani mimi/ Nilichohitaji.. ni kuitumia hii sanaa ili nishee na nyinyi/ Hii zawadi.. niliyopewa na MPAJI ninayemuamini/ MPAJI aliyenivika taji ilimradi incharge ni win/ Na ninaamini.. kuna muda huongea kwa kupitia mimi/ Na hunisamehe ninapokosea.. ni vyema mkanizoea nyinyi/ Naweza kuona unachotaka au atakachonionyesha/ Nikitoa ngoma.. wanaitaka.. wanaipata.. coz wewe ni special Chorus: Mimi na wewe.. tangu long time/ Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame/ Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream… BONGO HIPHOP X2