Fid Q - 13 lyrics

Published

0 684 0

Fid Q - 13 lyrics

Intro: Hahahhaa 13 Bongo Records.. [Verse 1: Msodoki] Mama ndiye alinitabiri mi nitakuwa staa na nyota kila pande Nikiwa na raha, kama nina hasira nisijigambe Usimpige mkeo, piga shangwe! Maana Young k**a sio ngazi, kwa hiyo mwambieni shetani asinipande I think big, is my dream big kuwa bigga wa michano Ni**a ambae tajiri atanijua kuwa msodoki nawaficha mistari Upeo wangu umekula mchicha na ndiyo maana nna fikra za kuona mbali Msukuma naye sukuma mitikasi inatulia Hata Francis Cheka naweza mpiga punch akalia Wanayoijua njaa ndiyo wanaamini cha kwanza kilimo Mi sitaki gombania u-star ili nikifa nikazikwe kino Wabovu wakichana, imoo, na hawajui nguzo tano Leo kwenye u-star simo kisa sina muonekano Mi nna-power, ya ibada niliyo iomba baada ya kuipata Pole dada ulienitosa kisa umenizidi kidato Futa jasho na damu, saka noti, hali tete Watoto wanamjua Diamond na joti zaidi ya Kikwete Popote niko fiti, tega sikio Shoga hata akitoa jicho vipi, hawezi akayaona mafanikio ndiyoo [Hook: Belle 9, Fid Q & Msodoki] Msodoki na Ngoshaa Ndiyo miujiza iliyotabiriwa Haina haja ya kuogopa Nafasi nilizozichezea yawezekana zisirudi Lakini naweza zitengeneza nikiongeza juhudi Tangu Agosti, Tangu Aprili, 13 Tangu Agosti, Tangu Aprili, 13 Na-hustle bila wasi wala hofu Ubongo hauwezi nipa shida ambayo ntashindwa kuisolve [Verse 2: Fid Q] Wakishaamini unawahitaji zaidi ya wanavyo kuhitaji Mapenzi ya wadau wa mjini hugeuka samaki na maji Kuishi ndani yake tu, nje yake uvuliwe Kwa msaada wake upigwe, kisha anawishe uliwe Sikuumbwa nije ku-settle for less Naisubiri mvua inyeshe nijitokeze ku-dance Non sense sitemi, a**et siyo deni Homeboy, natema vitu on point, jifunzeni Thamini huu muda kabla hujageuka history Part of the past don't fit the script for the future memory Niliyo ya pitia yameniandaa kwa haya yajao Siyo dalili ya kusinzia, ni njaa nikipiga mihayo Sina jeuri wala mzaha kugeza tabia mbovu Nna kiburi cha jeraha ukinipoteza naacha kovu Maskini najiamini hadi natokwa na ukungu Bila ujuzi wasinge ni thamini ningetoswa mpaka na ndugu Kitacho nizamisha siyo kudondoka mtoni Ni kushindwa kupiga mbizi, nakusizi ili msinione [Hook: Belle 9, Fid Q & Msodoki] Msodoki na Ngoshaa Ndiyo miujiza iliyotabiriwa Haina haja ya kuogopa Nafasi nilizozichezea yawezekana zisirudi Lakini naweza zitengeneza nikiongeza juhudi Tangu Agosti, Tangu Aprili, 13 Tangu Agosti, Tangu Aprili, 13 Na-hustle bila wasi wala hofu Ubongo hauwezi nipa shida ambayo ntashindwa kuisolve [Verse 3: Fid Q & Msodoki] Fid Q: Napenda umaarufu, nachukia mbwembwe zake Unapospit truth kwa boothe afu wa-kush hamninyaki Nawaacha uchi, ukweli uzushi siyo mwake Hata mkighushi mtafeli hamnigusi na hamnipati Msodoki: Siamini nimekuwa mimi hadi leo nimefika hapa Alionilea hakuniamini, niliyemtegemea hakunitaka Bila nyinyi, wadau nakiri sishiki sarafu Na ndiyo maana sili bata, kwa maana bata wachafu Kuwa mkali wa kusifiwa, kubali kutumiwa Nilichoambiwa kuwa siku hizi hadi wajanja wan*liwa Inatakiwa kuwa streka, mambo yaende shkopa Kama hujanileta huwezi nirudisha nilipotoka Outro: Kumi na Tatu Kumi na Tatu Msodoki na Ngoshaa Tangu Agosti, Tangu Aprili, 13 Tangu Agosti, Tangu Aprili, 13