Erick Wainaina - Daima Kenya lyrics


Verse 1
Umoja ni fahari yetu
Undugu ndio nguvu
Chuki na ukabila
Hatutaki hata kamwe
Lazima tuungane, tuijenge nchi yetu
Pasiwe hata mmoja
Anaetenganisha Chorus
Naishi, Natumaini,
Najitolea daima Kenya,
Hakika ya bendera
Ni uthabiti wangu
Nyeusi ya wananchi na nyekundu ni ya damu
Kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani
Daima mimi mkenya
Mwananchi mzalendo Verse 2
Kwa uchungu na mateso
Kwa vilio na uzuni
Tulinyakuliwa Uhuru
na mashujaa wa zamani
Hawakushtushwa na risasi


au kufungwa gerezani
Nia yao ukombozi kuvunja pingu za ukoloni Chorus
Naishi, Natumaini,
Najitolea daima Kenya,
Hakika ya bendera
Ni uthabiti wangu
Nyeusi ya wananchi na nyekundu ni ya damu
Kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani
Daima mimi mkenya
Mwananchi mzalendo Verse 3
Wajibu wetu
Ni Kuishi kwa upendo
Kutoka ziwa Mpaka pwani
Kaskazini na kusini Chorus
Naishi, Natumaini,
Najitolea daima Kenya,
Hakika ya bendera
Ni uthabiti wangu
Nyeusi ya wananchi na nyekundu ni ya damu
Kijani ni ya ardhi, nyeupe ya amani
Daima mimi mkenya
Mwananchi mzalendo

Correct these Lyrics