Duke & Songa - Usiku lyrics

Published

0 1015 0

Duke & Songa - Usiku lyrics

[Verse 1: Songa] Natoka bush, naingia Dar Mataa yamejaa, kuona mwangaza naskia raha Nashuka kwenye ndinga naanza kumsaka uncle Nkilinda wajinga wasinpige changa la macho Nikamtafuta kila kona, haonekani Nkaingia kibanda cha simu, nikapiga simu hewani Samahani mteja unayempigia hapatikani Jaribu baadae, na kama ukishindwa hata mwakani Oh my God, ntafanya nini Wakati maskini na simjui yeyote hapa mjini Nkacheki mida, saa sita kasoro Pembeni nikaona giza, nkaanza kupita chochoro Vichaka vya ubungo, mashaka na mafumbo Mara nkasikia msaada vibaka wananipiga mtungo Sauti za chuki zikimfokea Nkasimama kutazama sauti inapo tokea Hook: Mi ni giza Kuna vingi vya kutisha Chunga sana pindi inapofika usiku Usiku, usiku, chunga sana pindi inapofika usiku Mi ni giza Kuna vingi vya kutisha Chunga sana pindi inapofika usiku Usiku, usiku, chunga sana pindi inapofika usiku [Verse 2: Songa] Nikashtuka kuona njemba zimejipanga Wawili wamemshika binti mwingine amebeba panga Akili ikacheza usoni kijasho chembamba Huku nkiwaza kwa hizi njemba nitaweza tamba Bila kusita nikainama nikaokota mawe Kurusha nikampiga mmoja la kichwa, wacha apagawe Wawili wakakimbia, mmoja ndio akabaki Akataka tuanzishe vita sijui ana roho ya ki-Gadaffi Nkaona poa, bila gumzo la kucheka Huyu bwege hanijui bush mi na tuzo ya mieleka Ngumi taekwondo hadi mafunzo yasiyo eleweka Pia nna ngumi kama nyundo huyu boya leo atabweka Nikarusha akakwepa, akarusha nikakwepa pia Nikamchota mtama, kuinuka akasepa na njia Kwakua ilikuwa giza, basi nikamwachia Akakimbia, huku binti akabaki an*lia Hook: Mi ni giza Kuna vingi vya kutisha Chunga sana pindi inapofika usiku Usiku, usiku, chunga sana pindi inapofika usiku Mi ni giza Kuna vingi vya kutisha Chunga sana pindi inapofika usiku Usiku, usiku, chunga sana pindi inapofika usiku [Verse 3: Songa] Nikamwambia binti usilie matatizo yapo Ila usiku kama huu kwanini unatembea peke yako Isitoshe we ni mrembo, upo shega balaa Kwa mavazi uliyovaa nahisi uliwatega jamaa Akasema, kwake huu ndio muda wa kazi Anauza mwili, ili apate mpunga wa malazi Nyumbani ana watoto Baba yao aliwakimbia, sababu ya wingi wa changamoto Anaganga na msoto Moto umetanda anashukuru japo hawana kitanda ila ana ndoto Mara akaanza kulia eti kaka unaroho ngapi Nikamwambia usilie mi ndio Songa nna roho safi Nakushauri sasa uende nyumbani Usiku usikukute hapa tena uende kwa amani Mshukuru sana Mungu kwa kukupa usicho kiomba Kwa sasa naondoka zangu naenda kumtafuta mjomba Hook: Mi ni giza Kuna vingi vya kutisha Chunga sana pindi inapofika usiku Usiku, usiku, chunga sana pindi inapofika usiku Mi ni giza Kuna vingi vya kutisha Chunga sana pindi inapofika usiku Usiku, usiku, chunga sana pindi inapofika usiku