Duke & Songa - Sorry lyrics

Published

0 993 0

Duke & Songa - Sorry lyrics

Intro: Tamaduni Muzik Yeah, Duke Tachez Songa [Verse I: Songa] Nilikwambia naitwa Harry, ukaniamini Nikaahidi kukujali ukiwa tayari kuwa na mimi Sikuwa muwazi kuhusu hali, nikadai siyo maskini Kwetu tuna nyumba na gari kuanzia bush mpaka mjini Nitakupa kupa raha, hujawahi pata Utang'aa mpaka hizo taa watazikata Huko uswazi ndio utasema sasa bye Utaponitaka, sitokuwa busy mithili ya jaffarai Kumbe nataka bupa kiroho safi Nikadai unahips kubwa mfano wa chupa ya konyagi Umenivuta nafsi Kwako nimekufa, na wala kufufuka sitaki Ni kama paka mwenye nguvu za panya Unawasi, we ni hasi unahitaji nguvu za chanya Nasikitika leo hujui cha kufanya I'm sorry, sitaki tena kukudanganya [Verse II: Songa] Mtoto kama Rambo kwenye scene Ukadata na mimi, ukawapiga chini Zaiid na Kibabu Wapoteen Baada ya bata za muda mfupi Ukahisi umepata bwana kumbe umepata nuksi Ukanipigia show, wala sikufanya booking Nini ice cream, kwangu ukalamba mpaka mkuki Ujuzi lukuki Sikuwa na muda wa kuhesabu magoli nilipiga tu mashuti Ki ukweli tuli-enjoy wasaa Tatizo ni kwamba nilikuona kama toy la mtaa Nikiacha sitoi, nikimwaga sizoi Ona sasa uko hoi balaa Ni kama paka mwenye nguvu za panya Unawasi, we ni hasi unahitaji nguvu za chanya Nasikitika leo hujui cha kufanya I'm sorry, sitaki tena kukudanganya [Verse III: Songa] Ki ukweli naitwa Songa maskini tu wakutupwa Hapa nilipo sina shillingi ya jinsi wala bukta Kipi nitakupa? Mi mwenyewe nimechacha mpaka nawaza lini nitakufa Vipi nitaondoa doa la ngozi Wallet kitunguu, nikifungua natoa chozi Sasa ni mchana na bado hujala Sikupi hela ya kusuka, siku hizi unanyoa upara Ni kipindi cha A,B,C Ila umechoka huna Mshindi wala HTC Ndiyo, mi ni real Emcee Lile gari niliazima tu kwa Willie HD Huh, tumuombe Mungu kwa sana Atupe imani, tuzishinde nguvu za ujana Nasikitika leo hujui cha kufanya I'm sorry, sitaki tena kukudanganya