Duke & Songa - Ndege lyrics

Published

0 894 0

Duke & Songa - Ndege lyrics

[Verse 1: Songa] Wengi wanaoskia zile sauti za ndege Huwa wanahisi ndege anaimba Lakini mi huwa sina mawazo ya kizembe Huwa nahisi labda ni kelele za shida Wamepatwa na wenge, au wanamsiba Au wanahitaji msaada mguu umechomwa na mwiba Au labda wameona mwizi akiiba Na hakuna mlinzi, kwa hiyo wanahitaji mchizi wakumpiga Pengine labda wameona ndege inapaa Wanashangaa, wanahisi ni jini mwenye pembe kadhaa Muda mwingine wanasali We utahisi hawalali, wapo tu ndani wanajivinjari Pengine ni msanii anamuita DJ Kwakua show haijaanza, wanapiga PA Usije pata mshangao wa kibwege Kaa na tafakari kumbuka hao ni ndege Hook: Unaweza kuwa unapiga mihayo Lakini kiziwi anayekutazama, akahisi tu unapiga kelele Ha, na huu ndio upande wa pili wa ndege Upande wa pili wa ndege Unaweza kuwa unapiga mihayo Lakini kiziwi anayekutazama, akahisi tu unapiga kelele Ha, na huu ndio upande wa pili wa ndege Upande wa pili wa ndege [Verse 2: Songa] Wengi wanaoskia zile sauti za ndege Huwa wanahisi ndege wan*lia Lakini mi huwa sina mawazo ya kizembe Huwa nakaa chini nafikiria Labda msitu ni mpya na wao wameingia Na hawana ndugu, hawajui wapi watafikia Wanapiga mihayo wengine wanasinzia Kiujumla wamechoka, kwa hiyo skia Kabla ya kusema pima Sijawahi skia ndege wamekamatwa na madawa ya kulevya china Kiafya wazima Na wanakata kiu japo hawajawahi chimba kisima Mabawa ndio nguzo Ya ndege nami kupitia wao ndio hivi nagawa funzo Sina cha zaidi kwako mzembe Nataka kukukumbusha kwamba hao ni ndege Hook: Unaweza kuwa unapiga mihayo Lakini kiziwi anayekutazama, akahisi tu unapiga kelele Ha, na huu ndio upande wa pili wa ndege Upande wa pili wa ndege Unaweza kuwa unapiga mihayo Lakini kiziwi anayekutazama, akahisi tu unapiga kelele Ha, na huu ndio upande wa pili wa ndege Upande wa pili wa ndege x2