Duke & Songa - Mwanga lyrics

Published

0 857 0

Duke & Songa - Mwanga lyrics

Intro: Duke Tachez, Songa, Tamaduni Muzik! [Verse I: Songa] Yea, Songa na Duke kazini Mungu nisamehe nafanya Rap, hizo __ mpe maskini Sasa mikosi mdosi kazeeka Nacheka, sishuki kama soksi za refa Hatari ni kuota moto sio ndoto Afadhali ni kumzaa mtoto sio choko Vocal sio ndogo Kama unatunza mazingira, inabidi ukate zogo sio gogo Bongo joto na michosho ya mwili Nakuacha wazi ka kicheche kwenye soko la mwili Kinachotoka kwenye ubongo ni siri Siku hizi sio uchizi, kuokota makopo ni dili Huh, nakupa falsafa za muziki Kwa vyombo vingi ka umezama maktaba ya mpishi Hali ilikikaba kwa dhiki Utabaki njia panda kama barnaba na pipi Hook: [Huu ni Mwanga umefika Kaa pembeni kama una nguvu za giza] x4 [Verse II: Songa] Naflow kama FISH Natoka Tamaduni, hakuna wa ku-flow kama sisi Kila rapper naemkuta juu ya mdundo, namtafuna Hadi mifupa, nina roho kama FISI Njoo kama PIMBI Uone jinsi nakukunja, nakurusha mi ni soo kwenye jiji Ukikimbia shoo, mi simo Mwana hara kati ka umeingia choo cha shimo Wanasema najua sana vitu Nimegundua kua mwezi ni kama jua la usiku Hakuna kama mi Wengi vichekesho ka Mzee Ojwaang na Mama Kayayii Chunga mapafu, vuta tumbaku Ichunguze afya yako kama umetumwa na udaku Navyotunga na ku-rap tu Wanasema nnalugha inayowavuta kama uga wa smaku Hook: [Huu ni Mwanga umefika Kaa pembeni kama una nguvu za giza] x8