Diamond Platnumz - Iyena lyrics

Published

0 527 0

Diamond Platnumz - Iyena lyrics

Hhhhmm! Ah! Leo Chereko chereko Mwanenu nimekuwa Zile kuringa mideko itapungua Ahsante mama ulinifunza nkajua Baba kasema kuomba mwiko Raha ya chumvi kununua Tena si kwa nazi Si hirizi za waganga Kwa baraka za baba na mama Tu na dua Waambie paparazi Pingamizi wenye viranga Waliosema hayawi hayawi yamekuwa Oooh! Oh! Iyena Iyena Iyena Iyena Iyena Iyena Kwaheri tutaonana Iyena Iyena (Aah ooh) Iyena Iyena (Aah Iyeena) Iyena Iyena Ntawakumbuka sana Ooh! Ndoa baraka Ukipata ushukuru Maana wanayoililia ni wengi sana Kwetu talaka Kuitoa ni kufuru Nimefunzwa vumilia Niushinde ujana Ili kesho mahususi Kusudi wasinong'one Embu nichumu niringe washushuke Na hii pete ya harusi Nakuvisha waone Wakale sumu Wavimbe wapasuke Eeh! Ati nashika nanga Nteke nsich*moke ndani (Anameremeta) Futa namba wablock vimada wa zamani (Anameremeta) Sio vijembe vya kanga waziwazi mambo hadharani (Anameremeta) Waliopanga mwenye nyumba kaja ndani (Anameremeta) Iyena Iyena (Aah iyoyo) Iyena Iyena (Aah Eeeh) Iyena Iyena Kwaheri tutaonana (Oh! Kwaheri Baba Mama) Iyena Iyena (Iyeeena) Iyena Iyena (Aah Eeh) Iyena Iyena Ntawakumbuka sana Imefika tamati Tulisubiri kitambo Leo samaki Kanasa kwenye chambo Pongezi kwa kamati Yanavutia mapambo Napata picha safi Litanikoma bundle Mwanamke usafi Gaga kulisugua Mume akirudi sharti Viatu kumvua Kitandani marashi Ma**age kumchua Kisha anza sayansi Viuno kutengua Mambo ya kuzima taa Si mahaba ni kuwanga Washa japo ka mshumaa Mumeo aone shanga Eeeeh! Makeup kinanda Kaka suit kama mbunge (Anameremeta) Mulo changa muda kujipooza na punje (Anameremeta) Momo ndani Shivo amekuja na Fumbwe (Anameremeta) Kula chanda ukishiba ruksa kafunge (Anameremeta) Iyena Iyena (Aah iyeee) Iyena Iyena (Aah iyoyo) Iyena Iyena Kwaheri tutaonana (Eh! Kwaheri Baba Mama) Iyena Iyena (Iyeee) Iyena Iyena (Hhhmm) Iyena Iyena Ntawakumbuka sana Saa nataka kusasambua (Sasambu) Me nasasambua (Sasambu) Aby Dad nasasambua mimi (Sasambu) Sasambua! Tuone Mguu moja juu (Sasambu) Usishushe chini (Sasambu) Cheza jitazame (Sasambu) Sasambua! Tuone Aisha kimobitel (Sasambu) Nipe za baloteli (Sasambu) Nyonga kibaiskeli (Sasambu) Sasambua! Tuone Akaa kama unashika ukuta (Sasambu) Ifanye unashusha (Sasambu) Taratibu zungusha (Sasambu) Sasambua Tuone Sasambu! Sasambu! Sasambu! Sasambua! Tuone Kama unawasha bajaji (Sasambu) Imwagie na maji (Sasambu) Tuwakomeshe vizazi (Sasambu) Sasambua! Tuone