Banana Zoro - Zoba lyrics

Published

0 3294 0

Banana Zoro - Zoba lyrics

Mafunzo yote! Pozi zote! Mauzo yote! Eti binti hanitaki Nimesubiri sana, nimechukua za uso, kuda deki! Si uzoba huu? Aiyey! Chorus Subira yangu ndiyo iliyoniponza Ngoja, ngoja, naonekana Zoba Subira yangu ndiyo iliyoniponza Ngoja, ngoja, naonekana mjinga Kwa sababu nilimpenda kweli (4x) Verse 1 Mawazo, mawazo yatawala kichwa changu, ee Maumivu, maumivu yamevunja moyo wangu ee Kusubiri, kusubiri, nimekusubiri mpenzi wangu ee Lakini umekuja kuuvunja moyo wangu ee Nilikuwa nikamili nisifanye jambo lolote nawe Mpaka tuje tufunge ndoa, umalize na masomo Huko umekwenda huko chuoni ee Umebadilika mama, umebadilika, umebadilika sana Mama yo, mama yo Mama yo, mama yo, mama yo Unaniona mimi Zoba, Zoo-oba ee Chorus Subira yangu ndiyo iliyoniponza (Imeniponza miye ee) Ngoja, ngoja, naonekana Zoba (Zoba la mapenzi ee) Subira yangu ndiyo iliyoniponza (Nimepotezwa miye ee) Ngoja, ngoja, naonekana mjinga (Sijui la kufanya ee) Kwa sababu nilimpenda kweli (Kweli eee) Kwa sababu nilimpenda kweli (Nilimpenda kweli) Kwa sababu nilimpenda kweli (Nilimpenda kweli ooo) Kwa sababu nilimpenda kweli (Mama yo, mama yo) Verse 2 Inauma sana, mpenzi wako Wampenda sana, wamlinda sana, Wapata habari, kumbe mwenzako Kampenda sana, rafiki yako Ndo maana juzi, umeacha mazoezi Ndo maana siku hizi hutaki kuwa na mimi Mapenzi (mapenzi) yananiumiza (yananiumiza) Mapenzi (mapenzi) yananitesa (nitakulinda wewe) Maumivi ya mapenzi, zaidi ya mwiba Sikitiko la mahaba, la shinda msiba Nitakulinda mama Nitafanya jambo lolote kwa ajili yako nahakikisha nakuwa na wewe, wewe ee Mama yo, mama yo, mama yo Unaniona mimi Zoba, Zoo-oba ee Chorus Subira yangu ndiyo iliyoniponza (Imeniponza miye ee) Ngoja, ngoja, naonekana Zoba (Zoba la mapenzi ee) Subira yangu ndiyo iliyoniponza (Nimepotezwa miye ee) Ngoja, ngoja, naonekana mjinga (Sijui la kufanya ee) Kwa sababu nilimpenda kweli (Kweli ee) Kwa sababu nilimpenda kweli (Nilimpenda kweli ee) Kwa sababu nilimpenda kweli (Nilimpenda kweli oo) Kwa sababu nilimpenda kweli Mama yo, mama yo (3x) Nitakulinda wewe, mpenzi wangu wewe Hii ni ahadi naiweka kwako wewe Wewe oo, wewe oo Upo kwa ajili yangu ee Nitasubiri siku zote Litunze penzi langu mama Mapenzi, mapenzi, mapenzi, mapenzi, mapenzi, mapenzi, mapenzi, mapenzi mabaya Mapenzi mabaya, mapenzi mabaya, mapenzi mabaya, mapenzi mabaya Lakini mpenzi wangu, mapenzi, umalize masomo tuwe wapenzi kweli Tufunge ndo na we mama nakupenda Nakupenda kama wali wa nazi (I love you) Mbona mwenyewe, Nimeamua kusubiri oo, kusubiri Usifanye mama, nikaonekana Zoba Nikija kungoja, siku zote mama