KiSwahili (verse:1) Ee Mungu nguvu yetu Ilete baraka kwetu Haki iwe ngao na mlinzi Natukae na udugu Amani na uhuru Raha tupate na ustawi. (verse:2) Amkeni ndugu zetu Tufanye sote bidii Nasi tujitoe kwa nguvu Nchi yetu ya Kenya
Tunayoipenda Tuwe tayari kuilinda (verse:3) Natujenge taifa letu Ee, ndio wajibu wetu Kenya istahili heshima Tuungane mikono Pamoja kazini Kila siku tuwe na shukrani Sent by Carlos Andr Pereira da Silva Branco