Verse 1(Kidum) Ikiwa umeamua kunitoroka ikiwa unahisi hujiskii nami tena na mbona imekuwa ngumu kunidokeza naona ni bora nilie leo, badala ya kesho kupenda, usipende ni kama kujitia kitanzi nitachimba na sururu kwa ardhi nikitafuta penzi lako ni heri nipigwe fimbo kwa mwili sababu ntajikuna ama ntajikanda na maji moto maumivu ya penzi, mtu hajikuni wala hajikandi na maji na hakuna upasuaji Chorus kama kuna kosa nimewahi fanya(nielezee) kama kuna jinsi tunaweza leta(mpaka niishi) na kama kuna kitendo linaweza tendwa(nielezee) nitafanya(fanya) nitatenda(tenda) nitafanya(fanya) nitatenda(tenda) nitafanya(fanya) nitatenda(tenda) nitafanya(fanya) nitatenda(tenda) Verse 2(Lady Jay Dee) kweli hukumbuki ulioyafanya ni kweli unakumbuka tulikotoka sisemi habari zozote za kusikia bali kwa ushahidi niliouona msamaha mara ngapi umeshaomba na bado chenye makosa mangapi niliyoyafumbia macho mpaka leo nahisi kufika kikomo maumivu yanazidi ndani ya moyo sitaki kwenda mbali kwani uko moyoni nikusamehe mimi mara ngapi wee nielezee mpenzi mara ngapi Chorus
unataka nikusamehe mara ngapi(usihesabu) ungependa nikuvumilie mara ngapi(hii ni ya mwisho) je wewe nikulilie mara ngapi(vumilia) sitoweza(utaweza wee) nimechoka(usichoke) nimeshindwa(usishindwe) naondoka(usiondoke) sitoweza(utaweza yee) nimechoka nimeshindwa(usishindwe) naondoka(usishindwe) Verse 3 ukihesabu mara ngapi umenisamehe ni kama kuhesabu ni mara ngapi mtoto kaharibu nappy usichoke usiondoke usilie niko hapa kukulinda Chorus kama kuna kosa nimewahi fanya(nielezee) kama kuna jinsi tunaweza leta(mpaka niishi) na kama kuna kitendo lingeweza tendwa(nielezee) nitafanya(fanya) nitatenda(tenda) nitafanya(fanya) nitatenda(tenda) nitafanya(fanya) nitatenda(tenda) nitafanya(fanya) nitatenda(tenda) unataka nikusamehe mara ngapi(usihesabu) ungependa nikuvumilie mara ngapi(hii ni ya mwisho) je wewe nikulilie mara ngapi(vumilia) sitoweza(utaweza wee) nimechoka(usichoke) nimeshindwa(usishindwe) naondoka(usiondoke) sitoweza(utaweza yee) nimechoka nimeshindwa(usishindwe) naondoka(usishindwe)