....yeah, thiz about life man.....(chiness bizness) Every thing you do, Fikiria, hujui place utaishia...au sio verse 1 Skiza story yake, mwana wa mabepari toka alipozaliwa hali yake ilikuwa shwari kama mtoto yeyote aliishi na wazazi na alipotak chochote alitegemea wazazi hizo hela za babake zilimpa ujeuri hakuna mtu yeyote aloweza kumshauri wote aliwachukua tu kama watu mabwege bila kujua hatimaye hali yake itakuwaje wazazi walimpenda mshkaji kaanza kudeka kajiona ameshafaulu shuleni akatoweka kajiunga na vikundi haram wakamchombeza mi nashindwa kwani hakufaham watampoteza? mshkaji alizidisha vituko kila kukicha leo kaiba mbuzi kesh okuku kamficha kapelekwa kwa chief, ili apate kumkashif, hapo bado kaishia kumtongoza mke wa chifu. Chorus Nilimuonya lakini hakusikia
aliona kama mimi siwezi kumsaidia cheki sasa hatimaye anajutia vitu alivofanya ndo sa' vinamchukia x2 verse 2 Zilipita siku chache hali ikizidi kuwa mbaya bwana chifu kampitisha kwenye koti za wilaya mateso aloyapata siwez kusimulia na mpaka siku ya leo bado nazifikiria alifanywa atembee huku amefungwa miguu wakamweka kwenye celi akisubiri siku kuu back at home, watu walishachoka naye mpaka wazazi wake walishachoka kuishi naye siku ilipowadia alipelekwa mahakamani kesi yake iliposikizwa alihukumiwa maishani cheki sasa anajuta, nafsi inamsuta kwani yeye ndo chanzo kwa yale yote yalomkuta sina uwezo wowote mie wa kumsaidia nilimuonya mara mia kaniona kama gunia so, peace for life, namalizia story yangu asiyefunzwa na mama hufunzwa na ulimwengu. chorus x2