AK47 - Kivyovyote lyrics

Published

0 247 0

AK47 - Kivyovyote lyrics

Verse 1: Huwa wanauliza na skiliza vipi, inapo skika beat Kwa hii mizani kwenye vina nashindwa ku-upima mziki Naposhika Bic, watoto wanashika speech Mi dondoko, Moko wa moto unamshika vipi? Chagua kujenga imani, au kujenga ghorofa Kumtenga mpinzani au ku-mpa ushindani wakutosha Chagua kupenda ku ghani sio kutoka Yaani, uzeekee ndani ya fani usipewe promo ya kutosha Unapovunjwa moyo, unaujenga tena Na usiweke chuki, iache iondoke na iende vyema Usimtenge mpendwa kwa moyo, umpende tena Usipende kusema tenda apendacho na utende vyema Milele ntasimama nikidondosha fasihi Wanabana kwakua nimekataa kuipotosha jamii Ila mkali naheshimika ki-uhakika sio kwa zali Na habari ikifika wataiandika kila mahali Hook: Kwa hiyo wanangu msichoke Niko on play, O.N.E kwenye kipaza, nkikaza usiogope Bwana its O.K, mi naifanya all day Hata wakibana mi naifanya kivyovyote Kwa hiyo wanangu msichoke Niko on play, O.N.E kwenye kipaza, nkikaza usiogope Bwana its O.K, mi naifanya all day Hata wakibana mi naifanya kivyovyote Verse 2: Sasa nimekua kijana wa makamo na sifa Napanga vyangu kwa mtazamo na mifano ya uhakika Jambo Afrika, nina jambo kwenye kichwa Kijana jenga msimamo kwani mahusiano huvunjika Moko sauti ya mtaa, uliza upate jibu Zaidi ya star, kivipi niende sawa na mawingu Mafanikio hafifu siyahitaji Kwani nlipo uanza mziki nlikuwa maskini mwenye kipaji Bado nipo town, chimbo underground mi napanga sound Bunduki kwenye mdundo utapagawa Wanataka niache ngumu nibane pua Ninyoe kiduku ndio niwe msanii wanaemtambua Ila, humu nilipo ndio unaponsikia Na kama haikushiki, hausiki, haitokusaidia Kule huku na njia Ila nacho sikia wasanii hawana stimu ka chupa tupu ya bia Hook: Kwa hiyo wanangu msichoke Niko on play, O.N.E kwenye kipaza, nkikaza usiogope Bwana its O.K, mi naifanya all day Hata wakibana mi naifanya kivyovyote Kwa hiyo wanangu msichoke Niko on play, O.N.E kwenye kipaza, nkikaza usiogope Bwana its O.K, mi naifanya all day Hata wakibana mi naifanya kivyovyote Verse 3: Wangependa wanifunge niwe mfungwa, nidundwe kama punda Ama SUGU, niwe bubu wanidhulumu mpaka lugha Ila bado sumu, uliza kisumu mpaka arachuga Navuna kigumu kwani hakuna mgumu wakuzivuna Nyingi pole kwa wazazi, habari shilole Ni majanga, waganga wanafiki ka walokole Wapole wangapi watanipa pole wakati Mi sina stori na wanafiki nawapa dole la kati Nichore wakati sina, nipore wakati nina Siwezi kuwa mpole kwa hawa wakore wanaoninyima Wanauliza vipi saa ngapi, kivipi wakati Hii ni hivi, wakuifanya hivi wako wapi? Skiiza, huu ni umahiri sio dharau Kwa huu ushairi utakumbuka usisahau Nipo town, nikimwaga sound kama spika Mshika dau, mi ndio dau lenye uhakika Hook: Kwa hiyo wanangu msichoke Niko on play, O.N.E kwenye kipaza, nkikaza usiogope Bwana its O.K, mi naifanya all day Hata wakibana mi naifanya kivyovyote Kwa hiyo wanangu msichoke Niko on play, O.N.E kwenye kipaza, nkikaza usiogope Bwana its O.K, mi naifanya all day Hata wakibana mi naifanya kivyovyote