Adam Shule Kongwe - Kurasa zilizokosekana lyrics

Published

0 162 0

Adam Shule Kongwe - Kurasa zilizokosekana lyrics

Verse 1: Africa Ni Taifa Sa Kwa Nini Waigawanye Wao Wametukuta Watakuaje Wafalme Hawa Wajinga Walijivisha Unadhifu Kisha Viongozi Wetu Wakawaita Ma Chief Wauaji Kama Leopold Kongo Mamilioni Ya Watu Walifukiwa Kwenye Udongo Sambamba Na Ukatili Kama Kukatwa Mikono Na Kutumikishwa Hakujafikaga Kikomo Migodi Ya South Vibarua Ni Wazawa Licha Ya Kazi Ngumu Walichukua Roho Zao Almasi Na Dhahabu Zenye Damu Mateso Mbalimbali Ya Mababu Kwenye Mashamba ------Mi Napata Moto Kwa Hakika Hasa Inapofika, Siku Ya Mtoto Wa Africa Kaburu Kutafuta Uhuru Kwani Kosa Nalilia Watoto Wa Kizulu Na Kikhosa Verse 2: Wanatuona Vibomba Hawa Jamaa Naskia Eti Papa Alishaomba Msamaha Nilishangaa, Huo Ni Upendo Wa Wapi Mnajua Mlipoteza Wazalendo Wangapi Itabadili Nini, Kivipi Mtatuambia Nini Saivi Kama Mama Africa Alidhalilishwa Vilivyo Kwenye Human Zoo Watoto Walilishwa Hadi Ndizi Hamuandiki, Mnatuongopea Achen Fix Badala Yake Mnatuletea Mafeminist Na Hadi Leo Mmebakisha Vinasaba Mkaleta Democrasia Kuzalisha Vibaraka Wa Umoja Wa Mataifa Au Umoja Wa Mataita Boda Za Bongo Hao Masoja Wataisha Mnawaua Wakati Nyie Mnashinda Ndani Na Mkuu Anajisifu Kusema Wan*linda Amani Verse 3: Tazama Mauaji Ya Wenyewe Kwa Wenyewе Power Ya Waasi Kusimama Vifua Mbele Silaha Za Kivita Na Kibaiolojia Dini Kutugawa Hadi Tunajichukia Wanapеana Vijiti Toka Karne Hii Kalamu Ni Zaidi Ya Mashine Ya Bomba Nane Na Popote Napowafuma Namimina Sijaganda Mawazo Ka Watumwa Wa Kifikra Usiniulize Kwamba Nani Namkolea Au Nani Noma Kati Ya Mmarekani Na Mkorea Huwezi Nikuta Namshabikia Trump Hawa Walete Acha Waikanyagie Track Mi Kioo Cha Jamii I Let The Freedom Ring Siwezi Sifia Wasenge Kama Kim Jong Ill Iko Wazi Watasiliba Ninavyotukana Kitu Wanachosifu Ni Jinsi China Inavyotufanya